Ugonjwa wa kisukari, kama jina linavyojieleza ni ongezeko la kiasi cha sukari katika damu. Ziko sababu nyingi zinazoweza sababisha ongezeko hili, ila kibaiologia ziko sababu mbili kubwa. nazo ni pamoja na mwili kushindwa kutengeneza insulin ya kutosha, au insulin inayotengenezwa kushindwa kufanya kazi ipasavyo. Kazi moja wapo ya insulin ni kusaidia sukari itumike katika kutengeneza nguvu miilini mwetu. Hivyo tatizo lolote la homoni hii iitwayo insulin, huweza sababisha sukari kuongezeka katika damu. Katika lugha rahisi tunasema kwamba, sukari ikiwa nyingi katika damu inakuwa kama sumu. Sumu hii huleta matatizo mengi yakiwemo matatizo ya macho, pamoja na matatizo ya mishipa ya damu na fahamu, ambayo huweza kusababisha magonjwa ya moyo au kudhoofika kwa nguvu za kiume.

Yako matatizo chungu nzima yatokanayo na sukari kuzidi katika damu, na tutakuwa tukiongelea tatizo moja moja ili upate kuelewa vema. Ujumbe muhimu katika andiko hili, ni swala la kuzingatia udhibiti wa kiasi cha sukari katika damu. Kama wewe una ugonjwa wa kisukari, hakikisha unafuata masharti yote uliyoelekezwa na daktari wako ili kuzuia sukari isiongezeke sana katika damu. Kwa kufanya hivyo unaweza kuishi maisha ya kawaida kama watu wengine. Kwa ushauri zaidi, usisite kuwasiliana nasi. Tuma maswali na maoni yako, na sisi tutakuwa tayari kabisa kukusaidia.
 
 
 
 
Katika Baadhi ya jamii zetu za kiAfrica, Unene na kitambi ni fahari. Inaonyesha uwezo wa mwanaume kuitunza familia yake na pia umahiri wa mwanamke katika kupika. Sehemu nyingine huonekana kama hali ya kuwa na afya nzuri. Kwa maana hiyo ni vema kufahamu madhara ya unene uliokidhiri kwa afya zetu.
In some of the African societies, obesity and belly fat are still regarded as signs of well being. It reflects  men's financial power and the adroitness of women in cooking. In fact in some places it even reflects good health. It is therefore important to be aware of the obesity related health problems.
 
 
Unaswali lolote kuhusu unene, ugonjwa wa kisukari au matatizo mengine yoyote yanayohusiana na na unene na kisukari? TUPO KWA AJILI YAKO
Do you have any question on obesity, diabetes or any other obesity and diabetes related problem? Feel free to ask, WE ARE HERE FOR YOU
 

    Dr Fredirick Mashili

    A medical doctor, scientist, author, educator and illustrator.

    Daktari, mwanasayansi, mtunzi, muelimishaji na mchoraji.

    In this blog you will benefit from relatively simplified health information on diabetes and obesity related diseases

    Katika blog hii utafaidika na maelezo na vielelezo rahisi kuhusu ugonjwa wa kisukari na matatizo yanayoambatana na unene uliokithiri.

    Archives

    September 2012

    Categories

    All

    View my profile on LinkedIn